Neno | Iringo SDA Choir

Chief

Chief of Sinners.

Neno - Iringo SDA Choir - Lyrics​

(Niko hivi kwa sababu ya neno, neno la Mungu
Neno la Mungu ni nuru imulikayo gizani
Neno ni mwanga wa njia yangu, huniongoza nisijikwaye
Nipe biblia neno litokalo kinywani mwa Mungu) x2

(Naipenda biblia yangu chuo cha mbinguni
Uipende biblia yako itengee muda
Tazama mwovu alivyofaulu wewe utingwe usipate muda
Hata kidogo kusoma neno, turejee chuoni mwake Mungu
Katika biblia Mungu hunena na roho zetu (kwani)
Humo chuoni taa zetu zitajazwa mafuta tele) x2

(Twaweza kusoma gazeti kurasa zake zote tusisinzie
Twaweza tazama mikanda na picha za hadithi tusisinzie
Adui ajua ndani ya biblia kuna hazina za kiroho
Watoto wa Mungu tuamke tuzitwae biblia zetu
Napenda biblia yangu ipende biblia yako tutenge muda tusome
Tuyarudie mapito ya kale, neno la Mungu tulisome
Neno linaonya labadilisha, siku kwa siku soma maandiko)
x2

(Utajiri wa kiroho u katika neno
Macho yatafunguliwa tusomapo neno
Akili zetu zimeshikiliwa, nazo hadithi pia maigizo
Zipinge hila zake mwovu, biblia tu iwe mwalimu wako
Uyatafakari matendo makuu na miujiza (kweli)
Visa vizuri vyafundisha namna ya kushinda dhambi) x2

(Twaweza kusoma gazeti kurasa zake zote tusisinzie
Twaweza tazama mikanda na picha za hadithi tusisinzie
Adui ajua ndani ya biblia kuna hazina za kiroho
Watoto wa Mungu tuamke tuzitwae biblia zetu
Napenda biblia yangu ipende biblia yako tutenge muda tusome
Tuyarudie mapito ya kale, neno la Mungu tulisome
Neno linaonya labadilisha, siku kwa siku soma maandiko)
x2

Neno - Iringo SDA Choir - English Lyrics​

(I am like this because of the word, the word of God
The word of God is the light that shines in darkness
The word of God is the light of my path, it guides me not to stumble
Give me the bible, the word that comes from the mouth of God) x2

(I love my bible, the college of heaven
Love your bible, set time for it
See how the wicked one has prospered, that you should not have time
At all to study the word, let's return to God's college
In the bible God speaks to our souls (for)
Therein our lamps will be filled with plenteous oil) x2

(We can read all the pages of the newspaper, and not fall asleep
We can watch tapes and pictorial stories, and not fall asleep
The enemy knows that in the bible, there are spiritual treasures
Children of God, let's wake up and pick our bibles
I love my bible, love your bible; let's take time to read
Let's recourse the ancient passages, the word of God let's read it
The word that warns and transforms, day by day read the scriptures
) x2

(Spiritual wealth is in the word
Eyes will be opened when we read the word
Our minds are engrossed in stories and dramas
Resist the tricks of the evil one, only the bible your teacher be
Reflect on the great deeds and miracles (surely)
Good parables teach how to overcome sin) x2

(We can read all the pages of the newspaper, and not fall asleep
We can watch tapes and pictorial stories, and not fall asleep
The enemy knows that in the bible, there are spiritual treasures
Children of God, let's wake up and pick our bibles
I love my bible, love your bible; let's take time to read
Let's recourse the ancient passages, the word of God let's read it
The word that warns and transforms, day by day read the scriptures
) x2
 
Last edited:
Back
Top