Rangi | Ambassadors of Christ

Chief

Chief of Sinners.

Rangi - Ambassadors of Christ - Lyrics​


Rangi zipo nyingi, Duniani
Tena zote ni rangi nzuri, Zapendeza
Ipo nyeupe nyekundu na njano (Zote), Za kupendeza sana
Tena nyeusi na rangi ya chenza, Kijani na kadharika
Japo zote nzuri, Zapendeza
Sio zote zawezafaa, Kwa wakati mmoja
Mtu mmoja kwa mapenzi yake, ataichagua rangi furani
Atakayojisikia ya mpendeza, Kuliko zile rangi nyingine
Chunga usijifanye mjanja, Kwa machaguzi yake
Ukisema rangi ni rangi, Yoyote yawezafaa
Vivyo hivyo mwenyezi Mungu, Kaitenga siku ya saba
Iwe ni sabato kwake, Pia kwa watu wake
Kwa nini nijifanye mjanja, Nikisema siku ni siku
Ndio siku zote ni nzuri, Lakini ya saba bora kwake

Nitawafundishaa,Watu kupumzika
Siku ya sabato, Kama alivyotuagiza Mungu
Nitawakumbushaa, Wote kupumzikaa
Siku ya sabato, Kama alivyotuagiza Mungu


Mataifa yetu mbalimbali, Yanazo bendera zake nzuri
Wote twaziheshimu
Zipo rangi zilizochaguliwa, Kuzipamba hizo bendera
Nyengine nyeusi na kijana, Nyekundu na kadhalika
Jee itakuwaje siku moja, Mtu mmoja kujifanya mjanja
Na kuzibadili rangi
Pale palipo rangi ya kijani, Yeye akaweka nyekundu
Tena palipo na njano, Yeye akaweka nyeupe
Ndivyo akasema rangi ni rangi, Hiyo nayo ni bendera tosha
Tafakari sana
Bila shaka mtu kama huyo, Atahukumiwaaa
Kwa kutoliheshimu taifa lile, Pia na bendera yake
Vivyo hivyo atahukumiwa, Mtu ajifanyaye mjanja
Kwa kusema siku ni siku, Ya saba sio bora sana
Vivyo hivyo mwenyezi mungu,Kaitenga siku ya saba
Iwe ni sabato kwake, Pia kwa watu wakee
Kwanini nijifanye mjanja,Nikisema siku ni siku
Ndio siku zote ni nzuri, Lakini ya saba bora kwake
 
Last edited:
Back
Top