Tuinue Mioyo | Iringo SDA Choir

Chief

Chief of Sinners.

Tuinue Mioyo - Iringo SDA Choir - Lyrics​

(Tuinueni mioyo sote pamoja tuimbe wimbo, wimbo wa utukufu za sifa kwa Mungu baba
Alinena ikawa mbingu na nchi na vijazavyo, alituumba sisi kwa namna ya ajabu
) x2

1.
Kazi zake ajabu mbunguni angani duniani, bahari maziwa mito milima nayo mabonde
Mungu mwingi wa fadhili mfalme wa wafalme, wewe u wa milele twapaswa kukuabudu

(Tuinueni mioyo sote pamoja tuimbe wimbo, wimbo wa utukufu za sifa kwa Mungu baba
Alinena ikawa mbingu na nchi na vijazavyo, alituumba sisi kwa namna ya ajabu
) x2

2.
Wanadamu wamejitukuza wapo kwa kitambo, astahilie utukufu ni Mungu pekee
Umetmalaki mwenyezi kila goti lisujudu, kila kiumbe sifu mataifa shangilia

(Tuinueni mioyo sote pamoja tuimbe wimbo, wimbo wa utukufu za sifa kwa Mungu baba
Alinena ikawa mbingu na nchi na vijazavyo, alituumba sisi kwa namna ya ajabu
) x2

3.
Astahili kuabudiwa muumbaji mfalme mbinguni na duniani ametamalaki bwana
Enzi zote za dunia ameziweka mwenyezi na atazikomesha, kisha ataleta ufalme wake wa milele
Tumfanyie shangwe tupa-aze sauti kila mtu na aseme Mungu wetu yu mwema, atupaye riziki afya pia uzima

(Tuinueni mioyo sote pamoja tuimbe wimbo, wimbo wa utukufu za sifa kwa Mungu baba
Alinena ikawa mbingu na nchi na vijazavyo, alituumba sisi kwa namna ya ajabu
) x2
(Kila nafsi imba Yehova ni bwana, yeye yule jana leo na milele
Atukuzwe Mungu mweza wa yote, tumshangilieni tumpee sifa
} x2
 
Last edited:
Back
Top